Rais wa Iran Ebrahim Raisi amezishutumu nchi za magharibi kuhusiana na misimamo yao ya kukumbatia vitendo vya ushoga, kauli ambayo ameitoa wakati akiwa katika ziara yake nchini Uganda.
Raisi ambaye yupo katika mpango kuimarisha ushirikiano, ikiwa
ni safari ya kwanza kwa kiongozi Irani Afrika katika miaka 11, ametoa wito huo akiwa
na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni.
"Mataifa ya magharibi yanajaribu kuhamasisha mawazo ya
ushoga pamoja na kuhamasisha ushoga, wanajaribu kumaliza kizazi cha binadamu
duniani," alisema Rais Raisi.
Rais Museveni alitia saini kuwa sheria muswada wa sheria ya
kali ya kupinga ushoga Mei 29, na kuibua kauli za kulalamikiwa na makundi ya
haki za binadamu, Umoja wa Mataifa, wanaharakati wa LGBTQ na mataifa ya
Magharibi.
0 Maoni