Power Tiller lakatisha uhai wa Mbunge wa Mbarali

Mbunge wa Jimbo la Mbarali Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Francis Leonard Mtega amefariki leo mchana kwa ajali ya pikipiki pikipiki akiwa anaelekea shambani kwake.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amesema Mtega amefariki kwa ajali ya pikipiki iliyokuwa imembeba ambayo imegongana na trekta aina ya power tiller.

Homera amesema mwili wa mbunge huyo umeondolewa katika Hospitali ya Chimala na kupelekwa Hospitali ya Rujewa ambayo inahuduma la jokofu la kuhifadhia maiti.



Chapisha Maoni

0 Maoni