Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel
Chongolo amekutana na kufanya mazungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan
Patriotic Front (RPF – Inkotanyi) Ndugu Wellars Gasamagera leo tarehe 1, Julai
2023 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF –
Inkotanyi) Mhe. Wellars Gasamagera aliasili nchini usiku wa kuamkia leo, kwa
ziara ya siku 5 na kupokelewa na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji
Ussi Gavu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa RPF – Inkontanyi
atatembelea kituyo cha televisheni cha Channel 10, mradi wa SGR pamoja na Shule
ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha kwa Mfipa.
0 Maoni