Ndege zisizo na rubani zashambulia uwanja wa ndege Moscow

 

Ukraine imeanzisha mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani (drone), Moscow, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema, na kulazimika kufungwa kwa muda moja wa uwanja mkubwa wa ndege wa nchi hiyo.

Ndege nne zisizo na rubani zimeripotiwa kutumika kufanya mashambulizi siku ya Jumanne, ambazo pia mashambulizi yake yamelenga eneo kubwa la Jiji la Moscow.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwamba ndege zote hizo zisizo na rubani zimetunguliwa na kuongeza kwamba hazikusababisha majeruhi yeyote.

Hata hivyo, nchi ya Ukraine haijathibitisha kuhusika na madai hayo ya Urusi ya mashambulizi.

Baadhi ya ndege zililazimika kubadilishwa muelekeo katika uwanja wa ndege wa Vnukovo katika kuepusha maafa, ingawa kwa sasa makatazo yameondolewa.

Chapisha Maoni

0 Maoni