Mkurugenzi Mkuu TTB amtembelea Balozi wa Uingereza kunadi utalii

 

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Damasi Mfugale amekutana na kufanya mazungumzo na Mh. Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bw. David Concar, katika kuendeleza programu ya kutembelea Balozi mbalimbali ili kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na masoko ya kimkakati ya utalii pamoja na masoko yanayoibuka,

Katika kikao hicho Bw. Mfugale na Balozi Concar wamejadili fursa mbalimbali za ushirikiano kati ya Bodi ya Utalii na Ubalozi wa Uingereza katika kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania kutoka Uingereza sambamba na kuvutia wawekezaji katika Sekta ya Utalii hususan kwenye maeneo ya kimkakati ikiwemo Kusini mwa Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni