Lissu aitwa polisi kwa kutoa maneno yasiyo na staha kwa Rais

 

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jina kutokana na kutoa maneno yasiyo na staha kumjibu Rais Samia Suluhu Hassan na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa nakala ya barua ya wito wa polisi ambayo Lissu ameiposti kwenye akaunti yake ya twitter maneno hayo ya Lissu yasiyo na staha kwa Rais Samia yalianza kusambaa mitandaoni kuanzia tarehe 15/07/2023.

Polisi wamesema ili waweze kukamilisha uchunguzi wao, wanamtaka Lissu afike kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jina, Makao Makuu Madogo ya Dar es Salaam siku ya Alhamisi tarehe 20, Julai 2023 saa 3:00 kamili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.



Chapisha Maoni

0 Maoni