Jecha hatosahaulika kwa uamuzi huu Rais Samia amlilia

 

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salum Jecha amefariki dunia, 


Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Naibu katibu mkuu CCM Zanzibar Mohamed Dimwa kuwa kifo chake kimetokea leo Jumanne, Julai 18, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Miongoni mwa matukio ambayo hayataweza sahaulika yaliyofanywa na Marehemu Jecha enzi za utumishi wake ni pamoja na kutangaza  kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi.


Oktoba 28, 2015 Jecha alitangaza maamuzi hayo   kupitia runinga ya serikali visiwani ZBC.

na kueleza kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi. 


Sababu alizotaja ni pamoja na kutuhumu  baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao.

RAIS SAMIA AMLILIA 

Kufuatia kifo chake Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia ndugu jamaa na marafiki na ameomba wanafamilia kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni