Dereva wa ajali iliyoua watu wanaofanya mazoezi akamatwa

 

Osward Kaijage mwenye umri wa miaka 39 mfanyakazi wa mgodi wa GGM Geita, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine kumi na sita katika ajali iliyotokea jumamosi wakati watu hao wakifanya mazoezi

Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Osward amekamatwa katika eneo la kisesa na bado anahojiwa na jeshi hilo na pindi upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani

Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa vikundi vyote vinavyofanya mazoezi ya mchakamchaka kujisajiri kwenye ofisi za utamaduni katika ngazi ya wilaya, manispaa na jiji ili wapate miongozi au maelekezo ya namna bora ya kufanya mazoezi kwa kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine

Chapisha Maoni

0 Maoni