Waasi wa ADF wauwa wanafunzi na kuteka wengine

 

Watu wapatao 40, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wameuawa wakiwa shuleni magharibi mwa Uganda, katika shambulizi lililofanya na waasi wenye uhusiano na kundi la Dola ya Kiislamu (IS).

Watu wengine zaidi, wanane wapo mahututi baada ya kufanyika kwa shambulizi hilo kwenye shule ya sekondari ya Lhubiriha iliyopo Mpondwe nchini Uganda.

Wanafunzi wa kiume wanaoishi kwenye mabweni ni miongoni mwa waliokufa, huku wengine kadhaa wakiwamo wanafunzi wakike wametekwa nyara na waasi hao.

Kundi la Allied Democratic Forces (ADF), lenye maskani yake katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia, limetupiwa lawama kwa kuhusika na shambulizi hilo shuleni.

Chapisha Maoni

0 Maoni