Ujerumani waendeleza uteja, wafungwa nyumbani

Wenyeji wa Euro 2024 Ujerumani, wamefungwa kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Colombia nyumbani, katika mchezo wa kirafiki.

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi iliyopigwa na Juan Cuadrado iliyompita Marc-Andre ter Stegen.

Cuadrado aliongeza goli la pili dakika za mwisho kwa mkwaju wa penati, baada ya Joshua Kimmich aliyetokea benchi kuunawa mpira.

Ujerumani baada ya kufungwa 3-2 na Ubelgiji mwezi Machi, walitoa sare 3-3 na Ukraine na kufungwa 1-0 na Poland mwezi huu.



Chapisha Maoni

0 Maoni