Sadio Mane aiongoza Senegal kuichakaza Brazil

 

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Sadio Mane amefunga mara mbili wakati Senegal ikiwachapa Brazil nagoli 4-2 katika mchezo wa kirafiki Lisbon, Ureno.

Kiungo wa West Ham Lucas Paqueta alikuwa wa kwanza kuipatia Brazil goli katika dakika ya 11 kabla ya Habib Diallo kusawazisha.

Goli la kujifunga la Marquinhos katika kipindi cha pili liliipatia Senegal goli la kuongoza huku Mane akiongezea jingine baada ya dakika ya 55.

Marquinhos alifunga goli la kusawazisha kwa Brazil lakini Mane alifunga goli lake la pili katika mchezo huo kwa mkwaju wa penati katika dakika za mwisho.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Estadio Jose Alvalade wa Sporting Lisbon, ambapo wachezaji tisa wa Ligi ya uingereza walishuka dimbani.

Chapisha Maoni

0 Maoni