Watu watatu akiwemo na mganga wa kienyeji aitwaye Ezekiel
Charles wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji ya mwanamke aliyejuliakana
kwa jina la Esther Lukonu mwenye umri wa miaka 51 wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina
Washtakiwa waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na Masunga
Mabula mwenye umri wa miaka 32, Ezekiel Charles mwenye umri wa miaka 40 ambae
ni mganga wa kienyeji pamoja na Salome Raphael mwenye umri wa miaka 32, ambao
wawsomewa kesi namba sita ya mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Amani
Mahimba wa Mahakama ya wilaya ya Magu Jijini Mwanza
Akiwasomea shtaka la mauaji linalowakabili Mwendesha mashtaka
wa Serikali mkaguzi Msaidizi wa polisi Chacha Msenye amesema mnamo tarehe kumi
ya mwezi watano mwaka huu washtakiwa hao wanadaiwa kumuua mwanamke aitwaye
Esther Lukoni kwa kumnyonga shingo kisha wakambaka na kumkata sehemu zake za
siri na mwili wake wakautupa kwenye shamba la mihogo.
Mahakama imeelezwa kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo
la mauaji kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu
sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama
hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shtaka hilo la mauaji na wamerudishwa rumande
katika gereza la wilaya ya Magu hadi tarehe 16 ya mwezi huu kesi hiyo
itakapotajwa tena.
Mganga wa kienyeji Ezekiel Charles katikati (mwenye nywele za afro) akiwa amekaa kwenye benchi Mahakamani pamoja na wenzake wawili walioshtakiwa kwa mauaji.
0 Maoni