Bunge lapitisha bajeti ya wizara ya fedha,Deni la taifa unafuu


 Wizara ya Fedha na Mipango imeomba ridhaa ya Bunge kuidhinisha Sh trilioni 15.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Shilingi trilioni 15.38 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 564.22 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, leo amewasilisha bungeni bajeti ya wizara hiyo makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kupitishwa na wabunge wa bunge hilo baada ya kujadiliwa kwa kina. Vipaumbele katika bajeti hiyo ni kama zinavyoonekana kwenye jedwali hapo chini;



Mchanganuo wa Bajeti ya Mafungu ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2023/24 kama unavyoonekana hapo chini.


DENI LA TAIFA 

Kuhusu deni la taofa Waziri dk Nchemba amesema  Wizara imelipa kwa wakati notisi za madai ya deni lililoiva la jumla ya shilingi trilioni 7.4.


Amesema Kupitia fungu namba 001, Bunge  liliidhinisha shilingi trilioni 9.1 kwa ajili ya kuhudumia deni la Serikali pindi linapoiva na hadi Aprili 2023, Wizara imelipa kwa wakati notisi za madai ya deni lililoiva la jumla ya shilingi trilioni 7.4 sawa na ufanisi wa asilimia 82 ya lengo.


“Kati ya kiasi hicho, deni la ndani ni shilingi trilioni 4.4 ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.7 na mtaji shilingi trilioni 2.7, aidha deni la nje ni shilingi trilioni 3, ikijumuisha riba shilingi trilioni 0.8 na mtaji shilingi trilioni 2.2”


“Wizara inaendelea kusimamia deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada ili  kuwa na taarifa sahihi kuhusu udhibiti wa deni la Serikali, Wizara  imefanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali kwa miaka 20 ijayo kuanzia 2022/23 hadi 2041/42”


Amesisitiza kuwa matokeo  ya tathmini yanaonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu, na  kuwa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.



Chapisha Maoni

0 Maoni