Bongozozo amuunga mkono Rais Samia

 

 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzanua(TTB), Damasi Mfugale amesema bodi hiyo ipo kwenye utekelezaji wa mikakati miwili ya utangazaji utalii wa Kusini mwa Tanzania kuanzia mwaka 2021-2026. 


Mfugale amesema   hayo Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha ziara ya utalii Kusini mwa Tanzania iliyofanywa na Balozi wa Hiari, Nicholas Reynolds maarufu kama Bongozozo kuunga mkono filamu ya: ‘Tanzania The Royal Tour’. iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Amesema mikakati hiyo imetaja njia za utangazaji wa utalii ikiwa ni pamoja na kutumia watu maarufu/mabalozi wa hiari, utangazaji kwa njia ya mtandao, vyombo vya habari, ziara za mafunzo na kushiriki katika maonesho ya kibiashara.


Bongozozo alifanya zuara  hiyo kuanzia Juni 12 hadi 24, 2023 katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania kwa kutembelea vivutio sita. 


Vivutio vilivyotembelewa ni pamoja na Hifadhi za Taifa za milima Udzungwa, Ruaha na Nyerere, pori la akiba la Mpanga Kipengere, kikundi cha utalii wa kitamaduni–Mtera Izazi na hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.


Mfugale amesema lengo la ziara hiyo ni kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Kusini mwa Tanzania ili kuongeza ufahamu na kuongeza idadi ya watalii.


“Pia kuleta ushawishi kwa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ambapo TTB ilifanya ubia na makampuni kutoka Kusini ambazo waliweza kuuza vifurushi na kuleta watalii ili kutalii na Bongozozo ikiwemo na vifurushi hivyo vilileta Watanzania 63 na Muingereza mmoja waliotembelea milima Udzungwa, Ruaha na Nyerere na pori la akiba la Mpanga Kipengere,”amesema Mfugale.

Chapisha Maoni

0 Maoni