Wasusia Waziri Mkuu kuzindua jengo jipya la Bunge

 

Waziri Mkuu Narendra Modi amezindua jengo jipya la Bunge la India huku kukiwapo na maandamano na migomo.

Wabunge wengi wa upinzani hawakushiriki uzinduzi huo, wakisema kwamba walitaka rais azindue jengo hilo la bunge na si Modi.

Katika maandamano hayo baadhi ya wanamieleka mashuhuri walikamatwa wakati wakikaribia eneo la bunge hilo jipya, kumpinga Modi.

Vyama vya upinzani India vimeikosoa serikali kwa kutomuomba Rais Droupadi Murmu, ambaye ndiye mkuu wa nchi, kufungua bunge hilo.

Baadhi ya waandamanaji wakiandamana kupinga Waziri Mkuu Modi kuzindua jengo jipya la Bunge India.

Chapisha Maoni

0 Maoni