Mahakama Kuu ya nchini Kenya, imeruhusu serikali kutwaa fedha shilingi milioni 102 za nchi hiyo alizohongwa mwanafunzi wakike mwenye umri wa miaka 23, Felista Nyamathira Njoroge, na mpenzi wake bilionea mzungu aishie nje ya nchi.
Katika hukumu iliyotolewa leo Mei 25 na Jaji Esther Maina,
serikali ya Kenya imeruhusiwa kukaa na fedha zinazoshikiliwa kwenye akaunti
mbili za benki zinazomilikiwa na Nyamathira baada ya kuelezwa zawadi hiyo ni
fedha zinazotakatishwa.
Jaji ameagiza kushikiliwa kwa fedha hizo ambazo ni sawa na
shilingi bilioni 1.7 za Tanzania kutokana na chanzo cha fedha hizo za bilionea Marc De Mesel, raia wa Ubeligiji anayejihusisha na sarafu pepe za
YouTube, hajaelezea malipo hayo na jinsi alivyozipata fedha hizo.
0 Maoni