Mmoja wa watu waliokimbia, kati ya watu wanne waliosalia ambao waliohusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda amekamatwa, Mwendesha Mashataka wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa amesema.
Mtuhuhumiwa huyo Fulgence Kayishema amekamatwa nchini Afrika
Kusini siku ya Jumatano, na waendesha mashtaka wameeleza kwamba anatarajiwa
kukabiliana na mashataka yake nchini Rwanda.
Kayishema ambaya alikuwa ni afisa wa polisi alishtakiwa
mwaka 2001 kuhusiana na tukio hilo, ambalo zaidi ya watu 2000, ambao ni wa
kabila la Watusi wanaume, wanawake na watoto waliuawa kwenye kanisa la Katoliki,
walipokuwa wamejihifadhi.
Watu wa kabila la Watusi 800,000 waliuawa wakati wa mauaji
hayo ya kimbari ya Rwanda 1994, pamoja na Wahutu wenye msimamo wa kati.
Kwa mujibu wa mashtaka Fulgence Kayishema, alihusika moja
kwa moja katika kupanga na kutekeleza mauaji ya wakimbizi waliojificha kanisa
la Nyange, lililopo Kivumu, Kibuye Aprili 15, mwaka 1994.
Katika mashtaka hayo imeelezwa Kayishema pamoja na wenzake
walijaribu kulichoma kanisa lililokuwa na watu walijificha kunusuru maisha yao,
na waliposhindwa wakaamua kuwavamia ndani na kuwashambulia kwa mapanga na
silaha zingine na kuwaua wote.
CHANZO: BBC
0 Maoni