Rais Samia atuma salam vifo vya watatu ajali ya ndege




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Watu watatu waliofariki katika  ajali ya ndege ya shirika la Frankfurt Zoological aina ya Cessna 182 na usajili wa namba 5H-FZS 


Ajali hiyo imetokea 5:30  muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka kwenye kiwanja kidogo cha Matambwe kwenye hifadhi ya taifa ya Nyerere, Ndege hiyo ilikuwa na abiria 3 na rubani 1.


Katika ajali hiyo askari wawili wamejeruliwa na hali zao sio nzuri ambapo baada ya kuokolewa walipokelewa katika zahanati wakisubiri ndege kupelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Majina ya waliofariki ni mtumishi mstaafu wa maliasili na utalii, Rubani Bernard Shayo, kutoka kampuni ya Frankfurt Zoological Society (FZS), Aman Mgogolo na askari mhifadhi Theonas Nota.


Miili ya marehemu imehifadhiwa katika zahanati hiyo, Rais Samia ametoa pole kwa familia za wafiwa na anaungana nao katika kipindi hiki cha majonzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili imeeleza Rubani Shayo pamoja na Mgogolo walifariki papo hapo, huku Askari Mhifadhi Nota, akifariki wakati ndege iliyokuwa ikimkimbiza hospitali kutua katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.


Chapisha Maoni

0 Maoni