Muhubiri ‘mbeba maono’ aliyetaka kukutana na Rais Ruto akamatwa


Polisi magharibi mwa Kenya, wamemkamata muhubiri mmoja ambaye hivi karibuni alisema anataka kukutana na Rais William Ruto ili  kumpatia maono ya kitume kuhusu hatma ya nchi hiyo.

Muhubiri huyo Joseph Chenge wa kanisa la Jerusalem Mowar amekamatwa jana jioni akiwa na waumini wake 11 katika kanisa lake lililopo Kijiji cha Ruri katika kaunti ya Homa Bay.

Afisa wa kitengo cha kuchunguza uhalifu Kenya Homa Bay, Bw. Abed Kavoo amesema kwamba wanamshikilia Muhubiri Chenge kwa tuhuma za kutoa mafundisho ya upotoshaji.

Bw. Kavoo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mhubiri huyo alikuwa anawazuia watu wagonjwa kanisani kwake kwa madai atawaombea wapone.

Wagonjwa watano wameokolewa kwenye kanisa hilo, katika zoezi lililofanywa na vyombo vya dola, nchini Kenya.

Polisi wamesema kanisa la Chenge linajiendesha kinyume na sharia, kwa kuwa halijaandikishwa. Muhubiri huyo pamoja na waumini wake wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani.

Chapisha Maoni

0 Maoni