Mwanamke IT ajichanganya akidhani kaombwa ngono na bosi

 


Mtumishi wakike wa kitengo cha IT huko London amemshtaki bosi wake kwa kumdhalilisha kingono, akiamini kuwa herufi “xx”, “yy” na “???” alizomtumia kwenye barua pepe ili kumpatia taarifa zaidi, ni ishara za kumuomba mahusiano ya mapenzi.

Mtumishi huyo wa kike Karina Gasparova pia amedai Mahakamani kuwa bosi wake huyo Alexander Goulandris amelipajina faili la kazini herufi ‘ajg’, ambazo ni kifupi cha maneno yanayomaanisha, uume mkubwa.

Mahakama ya kazi ya kati ya London, imesema kwamba mtazamo wa Bi. Gasparova kuhusiana na ufupisho wa herufi alizotumiwa na bosi wake ni potofu. Mahakama imeamua kutupilia mbali madai hayo.

Bi. Gasparova, alidai Mahakamani ‘xx’ inamanisha busu, ‘yy’ kuomba ngono na ‘???’ inamaanisha atakuwa tayari wakati gani wakafanye ngono.

Chapisha Maoni

0 Maoni