NDEGE iliyobeba wachezaji wa Yanga yashindwa kutua Dodoma yarejea Dar


Kikosi cha Klabu ya Yanga na msafara wake umerejea jijini Dar es Salaam baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kushindwa kutua katika uwanja wa ndege mkoani Dodoma.


Msafara wa kikosi cha klabu hiyo uliokuwa umesafiri mchana wa leo kuelekea Singida kwa kupitia Dodoma,

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema “Uongozi wa Yanga unapenda kuwatoa wasiwasi wanachama na mashabiki kuwa wachezaji wote na benchi la ufundi wako salama na hakuna tatizo lolote lililowakuta kutokana na changamoto hiyo”



Aidha, uongozi unaendelea na mipango ya haraka ya kuhakikisha timu inasafiri kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya kucheza mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars, uliopangwa kuchezwa Mei 4, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni