Mmoja afariki kwa Mkapa fainali ya Yanga Vs USM Alger


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema mtu mmoja amefariki dunia katika uwanja wa Benjamini Mkapa kutokana  msongamano wa mashabiki wakiingia uwanjani.

Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake mtandao wa Twitter  amesema kifo hicho kimetokea baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani na hadi sasa majeruhi ni 30 huku mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 40 amefariki dunia.



"Timu ya wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo standby kupokea na kuwahudumia majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi," ameandika Waziri Ummy.


Katika mechi hiyo ya fainali mzunguko wa kwanza ilihudhuriwa na mashabiki wengi licha ya yanga kutoweza kukata kiu kwa kuchapwa goli 2 kwa moja.

Chapisha Maoni

0 Maoni