Ukweli aliyejirusha ghorofani Makumbusho


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linachunguza tukio la kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Joel Misesemo aliyejirusha ghorofani Makumbusho.

Taarifa ya SACP Muliro imesema Misesemo mwenye umri kati ya miaka 35-40, mkazi wa Mwananyamala alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kinondoni na kufariki dunia.



Amesema Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alionekana katika jengo hilo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa 11:40 alifajiri na alimwambia mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, hata hivyo muda mfupi baadaye alijirusha kutoka juu ghorofani na kuanguka chini.


Aidha, mifumo ya kamera ya jengo hilo inamuonesha mtu huyo akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani, mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.



“Jeshi la Polisi limepata gari la marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na limehifadhiwa kituo cha Polisi Oysterbay, uchunguzi wa kina unaendelea juu ya tukio hilo” amesema SACP Muliro

Chapisha Maoni

0 Maoni