YANGA YAIBUGIZA RIVERS MAGOLI MAWILI KWA NUNGE




Klabu ya Soka ya wanajangwani Yanga SC imeibutua Rivers United ya nchini Nigeria kwa mabao mawili kwa nunge.


Mechi hiyo  ya kuwania kufuzu nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika imechezwa ugenini imeipa Yanga matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali wakati ikijiandaa na mechi ya marudiano nyumbani.


Magoli ya Yanga yote yamefungwa na Fiston Kayala Mayele katika kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya 0-0.



Huu ni muendelezo wa klabu  ya Wananchi kulipa kisasi cha kufungwa nje-ndani dhidi ya Rivers United katika kipindi cha mwaka 2021. 

Kwa sasa Yanga wanahitaji kumaliza shughuli kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 30, 2023 na kufuzu nusu fainali CAFCC.

MTANDAONI KWAFUKUTA

Miongoni mwa waliotoa pongezi ni Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia mtandao wa twita aliandika Hongereni watani wa jadi Simba na Yanga kwa ushindi katika michezo yenu ya CAF 



Mwingine ni Privadinyo ambaye meneja wa Digital wa Yanga alitoa ufafanuzi ushindi wa Yanga katika mechi zake za ndani na nje.

Chapisha Maoni

0 Maoni