Waumini waliokufa kwa kufunga hadi wafe Kenya wafikia 39


Miili mingine 18 ya watu imekutwa katika kijiji cha Shakahola nchini Kenya leo Aprili 23 majira ya mchana na kufanya idadi ya miili iliyopatikana tangu Ijumaa kufikia 39.

Zoezi la kufukua makaburi linaendelea katika eneo la Mchungaji Paul Mackenzie anayeshikiliwa na polisi, kwa kuwaagiza waumini wake kufunga hadi wafe ili wakutane na muumba wao.

Mwanamke mmoja ameokolewa katika eneo alilojificha akiwa amefunga na hali yake ilikuwa mbaya.

Mwanamke huyo ambaye alikuwa akielekea kufa aliwaashiria polisi kuwa hakuwa tayari kuokolewa asife.



Chapisha Maoni

0 Maoni