SIMBA YAICHAPA YANGA GOLI MBILI

Klabu ya Soka ya Wekundu wa Msimbazi wamechabanga Wanajangwani Yanga kwa goli mbili kwa bila na kujinyakulia point 3.


Mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam imekuwa ni ya malipizi katika historia ambapo Oktoba mwaka 1990 timu ya Yanga ilifunga Simba bao 3-0 wakiwa mabingwa watetezi.



Ushindi wa leo unaifanya Simba kusalia nafasi ya pili kwa point 63 dhidi bingwa mtetezi Yanga ambaye yupo kileleni kwa point 68, lolote linaweza tokea lakini Simba wanahitaji Point 5 ili kuweza kunusa ubingwa ambao imeupoteza kwa misimu miwili mfululizo.



Kwa sasa timu zote zinakabiliwa na mechi za Kimataifa ambapo Simba wanataraji kuumana na Wydad Casablanca katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, huku Yanga wakiwafuata Rivers United.


Chapisha Maoni

0 Maoni