Hizi ndizo sababu za Rais Samia kuwateua Diamond, Shilole kuwa pamoja na mawaziri, makatibu

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwimbaji na Staa Bongo Fleva Nchini Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz Pamoja na Msanii wa Kike na Mjasirimali Bi Zuwena Mohammed Shilole Kuwa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria Nchini. 


Taarifa kuhusu uteuzi huo imetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa afya Ummy Mwalimu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya malaria duniani alisema Baraza la Kupambana na maleria linaundwa na wajumbe 19 wakiwemo wasanii hao ikiwa ni mpango wa kuwafikia vijana ambao takwimu zinaonesha katika watu 100 watu 77 wana umri chini ya miaka 35.


Uteuzi Naseeb Abdul  maarufu Diamond Platnumz unatokana na kuwa  miongoni mwa vijana wenye ushawishi mkubwa nchini ambapo akaunti yake katika mtandao wa Instagram ina wafuasi milion 15.9 na uteuzi wake unawakilisha vijana ambao ni asilimia 73 ili kutoa ujumbe kuhusu kutokomeza malaria.


Msanii Shilole anawakilisha vijana kwa upande wa wanawake,ambaye ana wafuasi zaidi ya milion 9 wajumbe wengine ni pamoja na Faraja Nyalandu ambaye ni mkurugenzi wa ShuleDirect ambaye anasimamia mradi wa STEM yaani Sayansi Malaria na Mathematics na kuwa mchango wake utasaidia kutokomeza  malaria.



WENGINE WALIOTEULIWA 

Waziri wa Habari Mawasiliano na Tekinolojia  Nape Nnauye, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, Dk Hassan Abas, Wilson Mahera, Jimm Yonazi, Leodga Tenga, Mwenyekiti TPSF Angelina Ngalula, Simon Peter Shayo, Said Salim Bakhresa , Askofu Dk Fredrick Shoo, Mufti Aboubakari Zubeir, Askofu Gervas Nyaisonga (TEC) , Dk Hellen Senkoro Mkurugenzi Mkapa Foundation, Yang Kimaro Rais wa Klabu Ya Rotary.


Chapisha Maoni

0 Maoni