Kiza chatanda maziko ya watoto waliodaiwa kunyweshwa sumu na baba yao Chanika

 

Watoto wawili Abrahaman Kareem Chamwande na Kauthar Kareem Chamwande, waliodaiwa kuuwawa na baba yao kwa kunyweshwa sumu usiku wa Idd Pili wamezikwa.


Mazishi ya Watoto hao wawili yalifanyika usiku wa April 24 katika makaburi ya Kwa Mwarabu Chanika Mwisho ikiwa ni baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa miili ya watoto hao huku baba yao akishikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amesema jeshi la Polisi linamshikilia Kareem Chamwande anayedaiwa Kuwanywesha Sumu watoto wake watatu huko Kwangwale Chanika na kueleza jeshi hilo linaendela na uchunguzi kabla ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Awali Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Seif alithibitisha  ambapo alisema lilitokea majira ya saa 10 usiku wa kuamkia Idd Pili baada ya majirani kushtuka kuwepo na tukio hilo.

Seif akihojiwa na mwandishi wa TBC1 alisema kuwa alipopata taarifa alifika kuwaokoa watoto wakiwa na vyombo ulinzi waliwapeleka watoto hospitali ya Nguvukazi ambapo mtoto mdogo alifariki wakiwa njiani.


Kwa mujibu wa jirani Mohamed Ibrahimu ni jirani na nyumba ilipotokea tukio hilo alisema kuwa alipofika karibu na choo cha nyumba hiyo alisikia mtu akiwa kama anavunja miti karibu na choo alipochungulia ndipo alipomuona Kareem ambaye inadaiwa alitaka  kujiua kwa kutumbukia kwenye shimo la choo. 


Picha na Millardayo

Chapisha Maoni

0 Maoni