Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Kagame atakutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, IKULU Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Aprili 2023. Aidha, Viongozi hao Wakuu wataongea na Waandishi wa Habari kuelezea yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yao.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu ambapo nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kwenye sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo biashara na uwekezaji, nishati, uchukuzi, elimu na utamaduni. Kufanyika kwa ziara hii ni ishara nzuri ya kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa kidugu baina ya mataifa haya kwa maslahi mapana ya pande zote.
0 Maoni