Mhubiri wa wafuasi waliokufa njaa ajisalimisha

 

Mhubiri mtata Paul Makenzi wa kanisa la Good News International la Malindi nchini Kenya amejisalimisha polisi baada ya saa nne kupita tangu wafuasi wake wanne kufa njaa kutokana na mafundisho yake.

Mchungaji Makenzi amejisalimisha jana kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Kenya (DCI) Malindi wakati polisi walipofika Shakahola eneo la Chakama walipokufa wafuasi wake wanne na wengine kunusuriwa wasife kwa njaa kutokana na kufunga muda mrefu.

Mkutano wa dharura uliitishwa kwenye ofisi ya Naibu Kamishna wa Polisi Kaunti ya Malindi, ukiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi wa kaunti hiyo Angela Wanyama uliamua kutembelea eneo ambalo mamima ya wafuasi wa Mch. Makenzi inaaminika walikuwa wanafunga hadi wafe ili wakutane na muumba wao.

Kamati iliyoundwa kuchunguza tukio hilo la mhubiri huyo mtata inachunguza taarifa za kuwapo kwa kaburi walimozikwa watu wengi, huku Mhubiri Makenzi akitarajiwa kujibu mashtaka ya kupandikiza itikadi kali kwa wafuasi wake.

Operesheni iliyofanyika jana imefanikiwa kuwaokoa waumini wengine wanne wa kanisa la Good News International waliokuwa wamefunga hadi wafe na kupelekwa hospitali ya kaunti ya Malindi, na kuungana na wenzao 11 waliolazwa tangu siku ya Alhamis.

Mfuasi wa zamani wa Mchungaji Makenzi akiongozwa na viongozi wa baraza la kaunti ya Adu, Samson Zia ameshutumu mahubiri ya mchungaji huyo na kutoa wito kwa umma kuwa waangalifu na mahubiri hatarishi.

Wakati huo huo wachungaji wa Malindi, wamejitenganisha na mahubiri yenye utata ya mhubiri huyo, na kusema kwamba mahubiri ya Mchungaji Makenzi hayaendani na maandishi ya Mungu yaliyomo kwenye Biblia.

Akiongea kwa niaba ya waumini wa Kikristo Askofu James Njehia amesema kwamba imani ya Kikristo haishawsishi mtu yeyote kujiua kwa ajili ya wengine, tangu alipokufa Yesu Kristo kwa ajili ya kuwakomboa watu wote.

Askofu Njehia amewasihi ndugu wa wafuasi wa Mchungaji Makenzi waliojificha eneo la Shakahola wawatafute na kuwaokoa ili wasipoteze maisha, badala ya kungojea hadi watakapopoteza maisha na kupokea miili yao.

Chanzo: KBC


Chapisha Maoni

0 Maoni