Akizungumzia matokeo ya utafiti huo jijini Dar es Salaam Dk Palangyo amesema utafiti huo ulimhusisha kijana wa Kitanzania ambaye mshipa wake mkubwa wa moyo uliziba ghafla kwa asilimia 100.
“Unapokunywa kinywaji hiki huchukua muda wa dakika kumi hivi caffeine kuingia kwenye mzunguko wa damu, na matokeo yake mapigo ya moyo na shinikizo la damu huongezeka, hivyo kumwondolea mtu uchovu. Lakini ukizidisha hiki kinywaji inaleta athari kwenye mishipa,” alisema
Kwa mujibu wa utafiti huo ulibaini kijana huyo hakuwa na visababishi vyote vitano hatarishi ambayo ni mgonjwa ya kuambukiza, hakuwa mtumiaji wa sigara na pombe, hakuwa na uzito mkubwa, ulaji wake ulikuwa wa kawaida na mwenye kuzingatia mazoezi.
“Kitu pekee kilichobainika ni mtumiaji wa ‘energy drinks’ ambapo alikuwa kitumia makopo mawili hadi matano kwa siku”
“Na siku husika alikuwa ametoka kunywa makopo matano ndani ya saa nne. Baada ya kumaliza lile kopo la tano ndipo alipoanza kupata kichomi kwenye moyo, kiliendelea kuwa kikali pamoja na kwamba alimeza dawa za maumivu hakikutulia mpaka alipoletwa kwetu,” ameeleza Dkt. Palangyo.
Alisisitiza kwa jamii ya vijana kundi ambalo lipo hatarini haswa likiendelea na unywaji wa energy drinks linaweza kuzidisha wimbi la magonjwa ya moyo haswa ya mishipa ya moyo kuziba ambao wengi wao wapo chini ya miaka 45.TAKWIMU
Takwimu za mwaka 2021 zilizotolewa na JKCI zinaonesha takribani lita bilioni 25 za vinywaji vya kuongeza nguvu zilitumika duniani kote huku matumizi yakiongezeka kila uchwao.
MADEREVA DALADALA WAFUNGUKA
Kwa upande wao madereva wa daladala na makondakta katika jiji la Dar es asalaam wakihojiwa na Tbc1 walitoa shuhuda zao huku wengine wakieleza kuwa hawawezi kufanya kazi bila kunywa vinywaji hivyo.
Chanzo:JKCI/TBC1
0 Maoni