Kisiwa ‘kinachouzwa’ na mwekezaji ni mali ya TISEZA

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema imeona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa mwekezaji, Bw. Tim Draper, anakusudia kuuza ardhi katika kisiwa kilichopo Ziwa Tanganyika nchini Tanzania. 

Wizara hiyo imeutaarifu umma leo August 31, 2026 kuwa kisiwa kinachorejelewa ni Kisiwa cha Lupita, kilichopo katika Ziwa Tanganyika, Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa. 

Kisiwa hicho ni miongoni mwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji chini ya Mamlaka ya Uwekezaji na Usimamizi wa Maeneo ya Uwekezaji (TISEZA) na kimepangishwa kwa kampuni ya Firelight Safaris Ltd, ambayo Bw. Tim Draper, raia wa Marekani, ni miongoni mwa wanahisa. 

Kwa mujibu wa Wizara hiyo, Sheria ya Ardhi, Sura ya 113, imeweka utaratibu wa namna wawekezaji raia wa kigeni wanavyoweza kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji chini ya TISEZA. TISEZA, ambayo ndiyo mmiliki kwa mujibu wa sheria, imepangisha eneo hilo na kutoa Hakimiliki Isiyo ya Asili (Derivative Right) kwa kampuni ya Firelight Safaris Ltd kwa ajili ya matumizi ya hoteli ya kitalii. 

Hivyo, kampuni ya Firelight Safaris Ltd ni mwekezaji halali katika eneo hilo na inaweza kuhamisha uwekezaji wake kwa mwekezaji mwingine kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi, imeeleza taariza hiyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni