Kamishna
wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Abdul-Razaq
Badru ameongoza mbio za Fame Marathon zilizofanyika leo tarehe 14
Juni, 2026 katika mji wa Karatu mkoani Arusha.
Mbio hizo
zilizokuwa na umbali wa Kilomita 21, 10, 05 na 02 zimeratibiwa na
Hospitali ya Fame iliyopo Karatu na kuhusisha takribani wakimbiaji
650 kutoka ndani na nje ya Nchi.
Akizungumza wakati wa
Uzinduzi wa mbio hizo Kamishna Badru ameeleza kuwa Uhifadhi endelevu
ni pamoja na kushirikiana na Jamii zinazozunguka hifadhi katika
programu ambazo zina manufaa kwa Jamii na kutoa tabasamu kwa wagonjwa
mbalimbali wanaopata huduma kwenye Hospitali na Fame na nyinginezo
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Hospitali ya FAME Bw. William
Mhapa ameleeleza kuwa mbio hizo zinafanyika kwa mara ya tatu kwa
lengo kushirikiana na jamii kuchangia mahitaji mbalimbali ya wagonjwa
wanaofikishwa hospitali ya FAME kupata huduma za dharura na kutoa
msaada kwa jamii za Karatu, Ngorongoro na maeneo jirani.


.jpeg)
0 Maoni