Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa CRDB Bank Plc kutoka mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, Falme za Kiarabu na Rwanda wamerejea Nyumbani Ngorongoro
kushuhudia asili ya mababu zao iliyosheheni vivutio vya utalii vya
Wanyamapori, Malikale, Urithi wa Utamaduni na Jiolojia vilivyopo
Ngorongoro ambayo ni Kivutio bora cha Utalii Afrika mwaka 2023 na
2025.
Wakiwa ndani ya hifadhi hiyo maarufu duniani,
Wakurugenzi hao wamefurahishwa na mandhari, uoto wa asili,
wanyamapori pamoja na huduma bora za utalii zinazotolewa ndani ya
hifadhi na kusisitiza kuwa uzoefu walioupata umeacha alama
inayowafanya kurudi tena na familia zao.
Akizungumza kwa niaba
ya ujumbe huo, Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Prof. Neema Mori amesema
ujumbe huo umeichagua Ngorongoro kuwa sehemu yao ya mapumziko
kutokana na upekee wake usiofananishwa na eneo lolote duniani kwa
kuwa Ngorongoro si tu kivutio cha Utalii bali ni hazina ya historia,
utamaduni na asili inayoishi.
Akiwa na Ujumbe huo Kamishna
Msaidizi Mwandamizi anayesimamia Utalii na Masoko Mariam Kobelo
amesema kuwa Ngorongoro ndio eneo lenye ushahidi wa kisayansi na
Kimazingira kuwa binadamu wa kwanza alisimama kwa miguu yake miwili
zaidi ya miaka Milioni 3.6 iliyopita huku hifadhi hiyo ikipambwa na
wanyama wakubwa watano "Big Five", Spishi za Wanyama
mbalimbali, Ndege, maua na mimea.


.jpeg)
0 Maoni