Katika harakati za kuhakikisha amani ya nchi inadumu kwa muda mrefu, Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA kimeunga mkono mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande yanayotaka mabadiliko ya msingi katika mfumo wa sheria na utawala.
Katibu Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu amebainisha kuwa mahitaji ya Watanzania kwa sasa yamejikita katika kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa mwarobaini wa migogoro ya mara kwa mara.
Chama hicho kinaona kuwa kilio cha wananchi kuhusu hali ya uchumi na ajira kwa vijana ni viashiria vinavyopaswa kufanyiwa kazi haraka ili kulinda utulivu wa taifa.
Kwa kutambua kero hizi CHAUMMA inatoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti za kisheria ambazo zitatoa uhakika wa haki na usawa kwa kila raia bila kujali itikadi yake ya kisiasa.
Wakati
huo huo Chama cha Ukombozi wa Umma ( CHAUMMA) kimeeleza msimamo wake
kuwa maridhiano ya kweli ya kitaifa hayawezi kupatikana bila pande
zote zinazovutana kukubali kukaa pamoja na kuzungumza.
Katibu
Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu amesisitiza kuwa kukwepa mazungumzo
ni kuchelewesha utatuzi wa matatizo yanayoliyumbisha taifa hasa baada
ya matukio ya uchaguzi wa mwaka 2025.
Katibu mkuu huyo amesema CHAUMMA kimeridhika na vyanzo vya migogoro vilivyoibuliwa na Tume ya Jaji Chande na kwamba mazungumzo ni hatua ya kwanza kuelekea uponyaji wa nchi.
Chama hichokimesema kinaamini kuwa huu ni wakati muafaka wa kumaliza tofauti za kisiasa kwa kuweka maslahi ya nchi mbele ili kuepuka kurudia makosa yaleyale ambayo yamekuwa yakisababisha tume mbalimbali kuundwa bila ufumbuzi wa kudumu.
#MezaYaUmoja

0 Maoni