Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid, amesema kuwa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imefanya kazi kubwa na yenye tija kwa kuandaa ripoti iliyobainisha maeneo ambayo taifa lilifanya makosa na namna bora ya kusonga mbele kwa sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Hamad alieleza kuwa ripoti hiyo ni hatua muhimu katika mchakato wa maridhiano ya kitaifa, akisisitiza kuwa kila mwenye nia njema na taifa anapaswa kuweka kando tofauti zake.
Hamad radhi aliongeza kuwa ni wakati wa Watanzania kuunganisha nguvu, kutafuta suluhu ya changamoto zilizojitokeza, na kujenga umoja wa kitaifa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
#UmojaWetuNdiyoNguvuYetu
#turidhiane

0 Maoni