Hakuna Uhaba wa Bidhaa za Chakula Wafanyabishara Wasipandishe Bei - Dkt. Mwinyi

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hakuna uhaba wa bidhaa za chakula nchini, hivyo wafanyabiashara hawana sababu ya kupandisha bei wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo aliposhiriki Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Fatma Bint Issa, akisisitiza kuwa Ramadhan ni mwezi wa rehema na kusaidiana, si wa kuongeza bei za bidhaa za vyakula. 

Ameeleza kuwa Serikali imetoa maelekezo kwa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara kuhakikisha bei za mchele, unga wa ngano na sukari hazipandishwi, kwani zinapatikana kwa wingi. 

Aidha, amewahimiza Waumini kusaidiana na kuwasaidia wasio na uwezo, huku akiwataka wananchi kujiandaa vema kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Chapisha Maoni

0 Maoni