Sauti za wananchi walioathirika katika vurugu zilizoibuka hivi karibuni, zimeibua masuala
muhimu yanayohitaji utatuzi, ikiwemo maombi ya msaada, ushauri kwa vijana, na
pongezi kwa juhudi za Serikali.
Waathirika
wakizungumza nafasi ya Serikali katika kupoinya majeraha yao wameiomba
kuwaangaliwa waathirika wa moja kwa moja na uharibifu uliofanyika.
Mama Everina Mosses
Mmari, ambaye duka lake na mtaji wake wote viliungua, anaomba msaada wa
Serikali kumwezesha kurejea kwenye biashara. Aidha Benjamin, mfanyabiashara, anashauri
mamlaka husika kuendelea kuimarisha ulinzi katika jamii, akisisitiza kwamba
vurugu hutumiwa kama fursa ya kupora na kuharibu.
Hata hivyo, kuna
pongezi kwa vikosi vya ulinzi, huku Shaban Moshi Shaban akipongeza jitihada zao
za kurejesha utulivu na kuondoa changamoto.
Kwa upande wa ushauri
kwa jamii na vijana, kuna msisitizo wa kupunguza jazba na kutafuta njia sahihi
za kuwasilisha maoni.
Gaspar Apolnary
anashauri: "Sisi wenyewe tupunguze jazba, tufikishe maoni yetu. Wao
wanatupa mawaidha na sisi tutoe maoni kwa namna nyingine ila kwa kufanya fujo
inakuwa sio nzuri sana."
Anabainisha kuwa fujo
huathiri hata wale wasiohusika, mfano wagonjwa wanaoshindwa kupelekwa
hospitali.
Mama Everina naye
alisisitiza haja ya wazazi kukaa na watoto wao na kuwashauri maisha yanaendaje.
Kwa ujumla, ujumbe wa wananchi ni kwamba Tanzania imezoea amani na utatuzi wa
changamoto za kitaifa ni jukumu la wote kwa utulivu.

0 Maoni