Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa Mbobezi wa
Upasuaji wa Kurekebisha Taya kutoka nchini India, Dkt. Chirag Desai imeanza
kambi maalum ya kupandikiza meno kwa watu wenye changamoto ya kupoteza meno
kutokana na sababu mbalimbali.
Kupitia
kambi hiyo iliyoanza Oktoba 13, 2025 watu zaidi ya 40 watafanyiwa upasuaji wa
kupandikiza mzizi wa jino na wengine kupandikizwa meno bandia, kitu
kitakachowaweza watu hao kuondokana na hali ya ubogoyo waliyokuwa nayo awali.
Sio mara
ya kwanza kwa hospitali hiyo kufanya kambi maalum ya kupandikiza mzizi wa meno
na meno bandia kwani kambi hiyo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara ambapo kabla
ya kufanyika kwa kambi hii watu takribani 67 wameshanufaika na huduma hizo.
Kambi
hizi zinatumika kama jukwaa la kubadilishana uzoefu kati ya wataalam kutoka nje
ya nchi na watalaam wa ndani ili huduma hizo ziwe endelevu hapa nchini na
kuwapunguzia usumbufu wananchi kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hizo.
Kambi
hiyo ya kupandikiza meno itahitimishwa rasmi Oktoba 17, 2025, ambapo
inashauriwa wananchi wenye changamoto ya kupoteza meno kufika hospitalini hapo
kwa ajili ya uchunguzi na kupata matibu stahiki.

0 Maoni