Mgombea
mwenza katika kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amesema kuwa Serikali ijayo Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga
kuboresha sekta ya Uchukuzi mikoa ya kanda ya Kusini kwa kujenga meli mpya ya
mizigo ikiwemo kupanua Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, lengo ikiwa ni kuchochea
kasi ya ukuaji wa Uchumi kwa Wananchi.
Dkt.Nchimbi
ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 02, 2025 akihutubia maelfu ya Wananchi wa
Tandahimba waliofurika kumsikiliza wakati akinadi Sera na Ilani ya Uchaguzi ya
CCM ya 2025-2030, katika muendelezo wa mikutano ya Kampeni za Urais kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
"Nataka
niwaambie ndugu zangu kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) moja ya ajenda zake
muhimu ni kuhakikisha Sekta ya Uchukuzi inazidi kuimarika kwenye kanda hii ya
kusini, ambapo baada ya Kuingia Madarakani tutajenga meli mpya ya Mizigo ambayo
itasaidia kubeba Bidhaa kutoka hapa mtwara na kuzipeleka katika visiwa vya
Comoro ili kuwa na Soko la Uhakika," amesema Dkt Nchimbi.
Aidha,
Dkt.Nchimbi baada ya kuwahutubia Wananchi pia alipata fursa ya kuwanadi baadhi
ya wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la
Nanyamba,Ndugu Katani Ahmadi Katani pamoja na Madiwani.


0 Maoni