Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha kwa muda wa siku 90 Leseni ya Huduma za Maudhui Mtandaoni iliyotolewa kwa kampuni ya Vapper Tech Limited (JamiiForums) na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo.
Taarifa iliyotolewa na TCRA imesema imechukua hatua hiyo kufuatia kampuni hiyo kuchapisha kwenye mitandao yake ya kijamii maudhui ya kupotosha umma, kukashifu na kudhalilisha Serikali na Rais wa Tanzania kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni.
0 Maoni