Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
amepokea mkono wa pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha kaka yake, Abbas Ali Mwinyi,
kilichotokea jana tarehe 25 Septemba 2025.
Katika
kuonesha mshikamano wa kitaifa kwa familia ya marehemu Abbas Mwinyi, viongozi
mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan, walifika kutoa mkono wa pole nyumbani kwa familia Bweleo,
Mkoa wa Mjini Magharibi.
Miongoni
mwa walioungana na Rais Samia ni Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Mashaka Biteko,
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
Mwansasu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, pamoja na viongozi
wengine mbalimbali.
Marehemu atasaliwa Masjid Jamia Zinjibar, Mazizini baada ya Sala ya Ijumaa, na kuzikwa Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, leo tarehe 26 Septemba.




0 Maoni