Eneo la
kihistoria la Isimila Stone Age Site lililopo katika Mkoa wa Iringa, Tanzania,
limetangazwa kushinda miongoni mwa mawasilisho bora ya urithi na utafiti wa
pamoja kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Makumbusho (International council of
museums ICOM 2025) unaofanyika mjini Roma, Italia ulioanza 25-27/9/2025.
Ushindi
huo unaonesha thamani ya kipekee ya eneo la Isimila, maarufu kwa zana za mawe
yenye zaidi ya miaka 300,000, nguzo za asili na historia yake inayounganisha
mabara.
Aidha
wasilisho lililowasilishwa pia lilionesha uhusiano na mfanano wa Isimila na
Hifadhi ya Taifa Ruaha, ambayo imejaliwa vivutio vya kipekee vya nguzo za asili
maarufu kama Magda Natural Pillars.
Kupitia
mkutano huo, Tanzania imepata fursa ya kuyatangaza maeneo haya ya urithi
duniani kote, kuvutia watafiti wa kimataifa pamoja na wageni wa utalii wa
kiutamaduni na kihistoria.
Tanzania
kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inashiriki kuwasilisha
mchango wake wa kulinda urithi huo kwa njia ya ushirikiano, uhifadhi endelevu
na ushirikishwaji wa jamii.



0 Maoni