Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde ameendelea na
awamu ya kwanza ya kampeni yake ya mtaa kwa mtaa kwa kila kata kuzungumza na
makundi mbali katika maeneo husika.
Ndugu
Mavunde ameendelea na ziara yake kata ya IHUMWA na kutembelea na kuzungumza na
wananchi wa Mitaa ya Chang’ombe, Chilwana, Ilolo pamoja na Ihumwa.
Ndg.
Mavunde pia alitumia fursa hiyo kuwaombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM
Dkt. Samia S. Hassan na Mgombea Udiwani wa kata ya Ihumwa
Ndg. Edward Magawa.




0 Maoni