Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali
George Marwa Waitara amepokea tuzo ya kutambua mchango wake katika kuendeleza
na kusimamia shughuli za uhifadhi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14,
2025 na Mjumbe wa Bodi ya TANAPA Dkt. Robert Fyumagwa ambaye aliipokea kwa
niaba yake katika maadhimisho ya siku ya Askari Wanyamapori Duniani (World
Ranger’s Day) iliyoadhimishwa Julai 31,2025 katika Hifadhi ya
Taifa Tarangire.
0 Maoni