Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imenunua tiketi 500
kwa ajili ya kulipia mashabiki 500 kuingia uwanja wa Benjamini Mkapa leo tarehe
22 agosti, 2025 kwa ajili ya kushuhudia mechi ya robo fainali ambapo timu ya Tanzania -Taifa
stars itacheza na Morocco majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Benjamini
mkapa Dar es Salaam.
Akikabidhiwa tiketi hızo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi
wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Meneja wa idara ya huduma za utalii na
Masoko Mariam Kobelo amesema kuwa uamuzi wa kuingiza mashabiki hao 500 una
lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kuendeleza michezo na utalii pamoja
na kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
hususani hifadhi ya Ngorongoro.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msita ameipongeza NCAA kwa uamuzi huo
na kusema kuwa michuano ya fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)
imevuta mashabiki wengi katika nchi za
Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ni sehemu muhimu ya kutangaza vivutio vya
utalii.
Taifa stars na Morocco zitachuana ijumaa hii katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Na. Hamis Dambaya – Dar es Salaam
0 Maoni