Mwanariadha wa Italia afariki dunia China

Mchezaji wa mbio za kukimbia kwa ramani kutoka Italia, Mattia Debertolis, amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu wakati wa Michezo ya Dunia nchini China wiki iliyopita. 

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 alipatikana akiwa hana fahamu na waandaaji wa mashindano hayo siku ya Ijumaa iliyopita wakati wa tukio la orienteering huko Chengdu. 

Muitaliano huyo alifariki siku ya Jumanne, siku nne baada ya kuanguka.

 "Licha ya kupata huduma ya haraka na ya kitaalamu katika moja ya hospitali bora nchini China, alifariki dunia," waandaaji wa Michezo ya Dunia walisema katika taarifa yao. 

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mbio za Ramani (IOF), Tom Hollowell, alisema kuwa "hawezi kuelezea kwa maneno huzuni kuu isiyopimika kutokana na msiba huu mkubwa."

 Sababu ya kifo cha Debertolis haijafahamika hadi sasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni