Mbunge wa Jimbo la
Bukombe anayemaliza muda wake, Dkt. Doto Mashaka Biteko ambaye ameomba tena
ridhaa ya kutetea kiti hicho, ameeleza furaha na shukrani aliyonayo kwa
Wananchi wa Bukombe kufuatia ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita. @biteko
Dkt. Biteko amesema hayo
Agosti 2, 2025 kwa nyakati tofauti wakati akiomba kura kwa wajumbe wa Chama cha
Mapinduzi wa Kata za Lyambamgongo, Uyovu, Bugelenga, Katome, Igulwa na Runzewe
Mashariki zilizopo katika Jimbo la Bukombe.
" Mimi na viongozi
wenzangu wakiwemo wa vijiji na madiwani
ukianzia sekta ya Nishati tumesambaza umeme kila mahali, Sekta ya
miundombinu tumeongeza mtandao wa barabara kutoka km 259 hadi km 1,445 na Sekta
ya Elimu tunaongoza kwa kuwa na shule nyingi za Msingi na Sekondari tofauti na
ilivyokuwa Mwaka 2015 hatukuwa na shule ya sekondari ya upili hata moja lakini
mwaka 2025 tunazo shule TANO, Kwa upande
wa sekta ya afya tumepata miradi mbalimbali na fedha nyingi za kuboresha huduma
za afya katika wilaya yetu ya Bukombe”.
Katika hatua nyingine,
Dkt. Biteko amesema kuwa dhamira yake kwa Wanabukombe ni Maendeleo na wakati
wote anafikiria kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa Wananchi wote
"Moyoni mwangu ninalo deni kubwa sana la kufanya kazi zaidi kutokana na
heshima ambayo wananchi wameendelea kunipa wakati wote”. #Bukombe
#KusemaNaKutenda
0 Maoni