Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dustan Kitandula
ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kwa kufanya
tafiti za Misitu na Ufugaji Nyuki
zinazoleta tija na kutatua changamoto za wananchi.
Haya yamejiri hii jana Julai 07, 2025 katika Maonesho ya 49
ya Biashara ya Kimataifa SabaSaba ambayo yanaendelea jijini Dar es salaam,
baada ya kupata maelezo na elimu kutoka kwa mtaalam wa utafiti kuhusu uvunaji
wa miti kwa wakati kwa ajili ya mbao na utomvu unavyosaidia katika kukuza pato
la mwananchi lakin pia namna mkulima anatakiwa kuvuna kwa kuzingatia umri sahihi wa miti bila kupata hasara.
Aidha, Naibu Waziri Mhe. Kitandula amefurahishwa na tafiti
za ufugaji nyuki, hii ni baada ya kushuhudia utofauti wa rangi katika asali
unaotokana na aina ya mimea inayotumiwa na mdudu nyuki kutengeneza asali na
mazao mengineyo.
Pamoja na hayo, Mhe. Kitandula ameendelea kuwasisitiza
wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ili wapate elimu,
maelezo na kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana chini ya Wizara.
Ziara hii ya Mhe. Kitandula iliambatana na baadhi ya vipngozi wa Taasisi mbalimbali za wizara akiwamo Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo, Mkurugenzi Mkuu wa TTB Bw. Ephraim Mafuru, na Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI Dk. Revocatus Mushumbusi.
0 Maoni