Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa jana Julai 28, 2025 ameshiriki katika ufunguzi wa Jukwaa la nne wa
Kibiashara na Uwekezaji kati ya Afrika na Karibiani (Afri-Caribbean Trade and
Investment Forum - ACTIF 2025) mjini St. George’s, nchini Grenada, Julai
28,2025 ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo unaolenga
kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na visiwa vya
Karibiani umehudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka maeneo hayo.
0 Maoni